Hebrews 10:10-15

10 aKatika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.

11 bKila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi. 12 cLakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu. 13 dTangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake, 14 ekwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.

15 fPia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema:

Copyright information for SwhNEN